Aliyekuwa Mhasibu Msaidizi wa NSSF SACCOSS ashtakiwa kwa rushwa

DAR- Septemba 11,2024 shauri la uhujumu uchumi namba 26102/2024 kati ya Jamhuri dhidi ya Robert Stuart Konni ambaye alikuwa Mhasibu Msaidizi wa NSSF SACCOS Iimefunguliwa.

Ni mbele ya Hakimu Mheshimiwa Bittony Innocent Mwakisu wa Mahakama ya Wilaya Ilala mkoani Dar es Salaam.
Mshtakiwa ameshtakiwa kwa jumla ya makosa 311 yakiwemo; Kughushi, Kuwasilisha nyaraka zenye taarifa za uongo kinyume na kifungu cha 333,335(d)(i), 342 na 337 vyote vya Kanuni ya Adhabu, (Sura 16 Rejeo 2022).

Sambamba na kosa la Ubadhirifu na Ufujaji wa kiasi cha shilingi 338,172,694 kinyume na kifungu cha 28(2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, (Sura 329 Rejeo 2022).

Uchunguzi umethibitisha kwamba, mshtakiwa alidanganya na kuwezesha kulipwa, huku akijifanya ana ridhaa ya wanachama, mikopo mbalimbali kupitia hundi 144.

Mshtakiwa amekana makosa yote na kupelekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana aliyopewa.

Shauri hili ambalo lineendeshwa na waendesha Mashtaka Hassan Dunia na Gloria Mwainyekule, limeahirishwa hadi Septemba 25, 2024 kwa ajili ya kusomewa hoja za awali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news