Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yang'ara Maonesho ya Saba ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi

SINGIDA-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Taasisi za Fedha zilizoshiriki Maonesho ya Saba ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, yaliyofanyika kuanzia tarehe 8 hadi 14 Septemba 2024 katika viwanja vya Bombadier mkoani Singida.
Maonesho hayo yaliyoongozwa na kauli mbiu “Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Unufaike na Fursa za Uwezeshaji," yamehitimishwa rasmi leo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko.
Pia, Dkt. Biteko alipata fursa ya kutembelea banda la Benki Kuu na kupewa maelezo ya kina kuhusu namna Benki Kuu inavyosimamia mifuko ya udhamini wa mikopo kwa niaba ya Serikali.

Mifuko hii ni pamoja na Mfuko wa Udhamini wa Mikopo ya Mauzo Nje ya Nchi (Export Credit Guarantee Scheme - ECGS) na Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati (Small and Medium Enterprises Credit Guarantee Scheme - SME-CGS).
Lengo la mifuko hii ni kuwezesha wakopaji wa sekta binafsi na wenye upungufu wa dhamana na wanajihusisha na uzalishaji, kupata mitaji kutoka kwenye benki na taasisi za fedha ili kuchochea ukuaji wa uchumi kwa kuongeza uzalishaji, mauzo ya bidhaa nje ya nchi, ajira na mapato ya taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news