Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yatoa mafunzo maalum kwa wanachama wa VIDIWOTA jijini Mbeya

MBEYA- Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeendesha mafunzo maalum kwa wanachama wa Chama cha Wanawake Wenye Changamoto ya Ulemavu (VIDIWOTA) jijini Mbeya, yaliyolenga kuwasaidia kutambua alama za usalama kwenye noti na sarafu, kupata mikopo kutoka taasisi zinazosimamiwa na Benki Kuu, na kuelimishwa kuhusu uwekezaji katika dhamana za Serikali.
Kaimu Mkurugenzi wa Tawi la Benki Kuu Mbeya, Dkt. Nicholaus Kessy, alifungua mafunzo hayo yaliyofanyika katika Tawi la BoT Mbeya na kuhudhuriwa na wanachama 70 wa VIDIWOTA. Dkt. Kessy alisisitiza kuwa mafunzo hayo ni muhimu katika biashara zao, kwani yatawakinga dhidi ya udanganyifu wa kupokea fedha bandia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news