Bosi TCCIA kizimbani kwa uhujumu uchumi, ubadhirifu

NA DIRAMAKINI

ALIYEKUWA Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA),Bw.Gotfrid Mutagwaba Muganda amefunguliwa Shauri la Uhujumu Uchumi namba 27108/2024 na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Shauri hilo limefunguliwa Septemba 23,2024 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Mheshimiwa Anneth Nyenyema

Mshtakiwa ameshtakiwa kwa makosa mawili yakwemo Ubadhirifu na Ufujaji wa sh. 39,894,000 mali ya TCCIA pamoja na kosa la matumizi mabaya ya madaraka kinyume na kifungu cha 28(2) na 31 vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, (Sura 329 Rejeo 2022).

Aidha, shauri hilo lilitokana na tuhuma dhidi ya mshtakiwa kumpatia ajira Janeth Kambona kwa nafasi ya Msaidizi Binafsi wa Rais wa TCCIA huku akijua ni kinyume na utaratibu.

Hata hivyo, mshtakiwa amekana makosa yote na kupelekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana aliyopewa na shauri limeahirishwa hadi Oktoba 7, 2024 kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa hoja za awali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news