Bugando yapokea msaada wa mashine inayotumia mawimbi ya sauti

MWANZA-Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kupitia Idara ya Watoto Septemba 5, 2024 imepokea msaada wa Utra Sound Mashine mbili za kisasa kutoka Taasisi ya Ann & Robert Lurie Chidren Hospital ya nchini Marekani.

Hatua hiyo ni sehemu ya mashirikiano yaliyodumu kuanzia mwaka 2006 baina ya Hospitali ya Bugando na taasisi hiyo.
Msaada huo umepokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando,Dkt. Fabian Massaga, ambaye ameshukuru kwa msaada huo ambao unaenda kuboresha zaidi matibabu kwa watoto wa Kitanzania na Taifa na kusisitiza kuwa,

"Hospitali ya Bugando ni Hospitali ya kufundishia kama ilivyo Taasisi ya Ann & Robert Hospital,hivyo hii ni fursa kwetu kwani bado tunakua yunajilinganisha na ninyi, kupitia mashirikiano haya matamanio yetu ni kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo katika upande wa teknolojia mpya na ya kisasa katika masuala ya matibabu hususani matibabu ya moyo kwa watoto."

Kwa upande wake Dkt. Neema Chami, Mkuu wa Idara ya Watoto Hospitali ya Bugando mbali na kushukuru ameeleza kuwa,msaada huo utaondoa usumbufu wa kutegemea kipimo kimoja kwani uwepo wa mashine hizi mpya ambazo ni rahisi na zinahamishika zitasaidia sana matibabu.

Kwa upande wa wawakilishi kutoka Ann & Robert Lurie Children Hospital wamepongeza wataalamu kutoka Bugando kwa utayari wao wa kujifunza.

Aidha, Dkt. Julieth Kabirigi ambaye ni mnufaika wa programi hii amepongeza na kushukuru mashirikiano haya na taasisi hii kwa kutumia muda, pesa na kutanabaisha kuwa kwa kuwezesha mafunzo haya kutawasaidia watanzania walio wengi kutokana na ukweli kuwa unapofanya uchunguzi mapema ndivyo unapunguza hatari inayoweza kusababisha kifo kwa kugundua tatizo na kuwahi matibabu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news