Chagueni viongozi waadilifu-Naibu Waziri Pinda

MLELE-Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe. Geophrey Pinda amewataka wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuchagua viongozi waadilifu ambao hawataiingiza jamii kwenye matatizo yakiwemo yale ya Sekta ya Ardhi.
Mbunge wa Jimbo la Kavuu katika halmashauri ya Mpimbwe Mkoa wa Katavi na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza wakati wa Kikao cha Halmashauri ya CCM kata ya Majimoto wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi tarehe 26 Septemba 2024 katika Shule ya Msingi Majimoto.

Mhe.Pinda amesema hayo katika Kikao cha Halmashauri ya CCM kata ya Majimoto wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi kilichofanyika jana katika Shule ya Msingi Majimoto.

Amewaeleza wajumbe wa mkutano huo namna ambayo Wenyeviti wa Mitaa wanavyochangia migogoro ya ardhi jambo alilolieleza kuwa limetokana na kufanyika makosa wakati wa kuwachagua viongozi hao.
Sehemu ya wana CCM wakiwa katika kikao cha Halmashauri ya CCM Kata ya Majimoto Wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi tarehe 26 septemba 2024 katika Shule ya Msingi Majimoto.
"Huko Wizara ya Ardhi, jamani migogoro mingi ni ya wenyeviti kuuza maeneo bila ridhaa ya wananchi.

"Sasa tunaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ombi langu tukawapitishe watu kama mlivyonipitisha mimi na mimi nilivyowapitisha nyie kwa sifa zenu," amesongeza Mhe. Pinda.

Kwa mujibu wa Mbunge huyo wa jimbo la Kavuu, kiongozi bora ni yule aliye tayari kujitolea kwa moyo Kufanya kazi kizalendo kwa ajili ya wananchi wote nchini.
Mhe. Pinda amebainisha kuwa, kutokana na utendaji bora unaofanywa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi chini ya mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haoni kama kuna nafasi ya vyama vya upinzani kusimamisha mgombea.

Mhe. Geophrey Pinda yupo katika ziara jimboni kwake ambapo mbali na mambo mengine anatembelea kata zote ndani ya jimbo hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news