Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA), HAINAN kuendeleza uhusiano

ZANZIBAR-Ujumbe kutoka Chuo Kikuu cha Hainan nchini China tarehe 16 Septemba,2024 umekutana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Prof. Moh’d Makame Haji kwa mazungumzo ya kuendeleza uhusiano wa kitaaluma baina ya Vyuo vikuu hivi.
Katika mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi ya Makao Makuu ya SUZA huko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja, viongozi hao wamekubaliana kutiliana saini mkataba wa uhusiano baada ya kukamilika hatua za kisheria za hapa nchini.

Vyuo hivyo ambavyo vinatoa mafunzo yanayofanana na viko katika ukanda wa tropikali vitashirikiana katika masuala mbali mbali ya kukuza elimu, mawasiliano na kuimarisha kilimo.

Makamu wa Rais wa Chuo cha Hainan, Bw. Nie Qingbin, sote tuko katika ukanda wa kisiwa tuna miradi mizuri ya kuimarisha kilimo kama Zanzibar.

Wamependekeza ushirikiano katika kuwapatia kozi za muda mfupi na mrefu watendaji, kuimarisha kilimo, kubadilishana masuala ya utamaduni, mabadiliko ya hali hewa, ubaharia na utafiti.

SUZA kina mchango mkubwa katika kufanya tafiti za masuala ya bahari na mazingira ambayo nimuhimu katika wakati huu nchi inatekeleza sera ya Uchumi wa Buluu.
Aliongeza kuwa tafiti hizo zinafanywa kwa ushirikiano na baadhi ya Wizara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambazo zinahusiana na utekelezaji wa sera hiyo.

‘’SUZA kinatoa fursa kwa vyuo vya Tanzania kuja kufanya tafiti zao na kuleta matokeo mazuri, na kwa vile tuko tayari kwa kila mmoja kushirikiana nasi ili tuweze kufikia dhamira yetu ya kutoa elimu bora na tafiti kukabiliana changamoto zilizopo,’’alisema Prof. Haji.

Aidha, aliongeza kuwa amefurahishwa kuwepo ushirikiano huo katika kuwapatia mafunzo wafanyakazi wa SUZA, kushirikiana katika kufanya tafiti na pia akapendekeza kubadilishana utalaamu kwenye mafunzo ya lugha ya Kiswahili kwa Wachina na Kichina kwa wazawa.

Katika mazungumzo hayo, SUZA kimekubali kujiunga na Consotium of tropical Universities na kupokea mwaliko utakaovishikirisha vyuo hivyo hapo mwakani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news