DC mpya wa Mtwara akabidhiwa ofisi

MTWARA-Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Mwanahamisi Munkunda, Septemba 5,2024 amekabidhi Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara kwa Mkuu wa wilaya mpya, Mhe.Abdallah Mwaipaya.
Makabidhiano hayo yamefanyika kufuatia mabadiliko ya viongozi mbalimbali hapa nchini yaliyofanywa Septemba 3,2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Hafla ya makabidhiano imefanyika katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara yakishuhudiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya,

Viongozi mbalimbali wa dini na siasa, watumishi kutoka taasisi mbalimbali pamoja na wananchi.

Mhe.Mwanahamisi Munkunda kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news