ARUSHA-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini imetoa elimu kinga juu ya madhara ya matumizi na biashara ya dawa za kulevya kwa vijana 32.
Ni kwenye Jukwaa la Jioni ya Zamani lililofanyika eneo la Mji Mwema katika Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
Jukwaa hili ni mkusanyiko wa vijana ambao wameamua kukutana na kujadili mada mbalimbali ambazo zinahusu changamoto ambazo vijana wanakumbana nazo pamoja na fursa zilizopo.
Wakati wa uwasilishaji mada, afisa wa DCEA alizungumzia umuhimu wa malezi bora katika kupunguza tatizo la dawa za kulevya ambapo wazazi walihimizwa kufuatilia mienendo ya watoto wao ili kuweza kubaini mabadiliko ya tabia mapema kabla watoto hao hawajaingia katika matumizi ya dawa za kulevya.
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)