MTWARA-Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema kuwa dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha wananchi wananufaika na miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yao.

"Yote haya mnayoyaona ni matunda ya kazi nzuri ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye anaonesha kwa vitendo jinsi anavyowajali kwa kuhakikikisha mnapata huduma bora kupitia miradi hii,"amesisitiza Kapinga.
Ameeleza kuwa lengo la ziara hiyo ya Kamati ya Bunge ni kujionea thamani ya miradi hiyo ambayo itanufaisha wananchi wa Msimbati, ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko aliyoyatoa Novemba 15, 2024 mara baada ya kutembelea eneo hilo na kuzungumza na wananchi.

Kapinga amesisitiza kuwa, Serikali ipo pamoja na wananchi katika kuhakikisha inawapelekea maendeleo.
Katika hatua nyingine, Kapinga amewaasa wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa kwa kuanza kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.