Dkt.Gladness Ladislaus Salema achaguliwa kuwa Mbunge wa EALA

DODOMA-Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamechangua Dkt.Gladness Ladislaus Salema kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).
Ni kupitia uchaguzi ambao umefanyika Septemba 5, 2024.Dkt. Gladness ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam amechaguliwa ili kuziba nafasi iliyoachwa wazi na marehemu Dkt. Shogo Sedoyeka.
Dkt.Selema awali alinadi sera zake na kuomba kura kwa wabunge hao kabla ya kupigiwa kura
Aidha,amechaguliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kwa kupigiwa kura za ndiyo 254 na kura 18 za hapana kati ya kura 274 zilizopigwa na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news