Dkt.Yonazi ateta na uongozi wa Mpango wa Ulinzi wa Usalama na Utatuzi wa Mashambulizi (PSARP)

DODOMA-Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amekutana na kufanya mazungumzo na Mratibu wa Mpango wa Ulinzi wa Usalama na Utatuzi wa Mashambulizi (Protective Security & Attack Response Programme – PSARP) chini ya Ubalozi wa Uingereza kuhusu uwezekano wa kuandaa Mpango wa Kuimarisha Mfumo Jumuishi wa Usimamizi wa Maafa.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza na wageni kutoka Mpango wa Ulinzi wa Usalama na Utatuzi wa Mashambulizi (Protective Security & Attack Response Programme – PSARP) chini ya Ubalozi wa Uingereza kuhusu uwezekano wa kuandaa Mpango wa Kuimarisha Mfumo Jumuishi wa Usimamizi wa Maafa walipomtembelea Ofisini kwake tarehe 12 Septemba, 2024 jijini Dodoma.

Amekutana nao Septemba 12,2024 walipofika ofisi kwake jijini Dodoma, na kueleza kuwa PSARP ina lengo la kuimarisha uwezo wa wataalam katika kukabiliana na maafa nchini.
Mratibu wa Mpango wa Ulinzi wa Usalama na Utatuzi wa Mashambulizi (PSARP) - Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara Bw. John Spencer akizungumza jambo wakati wa kikao na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi walipomtembelea Ofisini kwake jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza na wageni kutoka Mpango wa Ulinzi wa Usalama na Utatuzi wa Mashambulizi (Protective Security & Attack Response Programme – PSARP) chini ya Ubalozi wa Uingereza kuhusu uwezekano wa kuandaa Mpango wa Kuimarisha Mfumo Jumuishi wa Usimamizi wa Maafa walipomtembelea Ofisini kwake tarehe 12 Septemba, 2024 jijini Dodoma.

Katika mazungumzo hayo, Dkt. Yonazi ameshukuru uongozi huo kwa kumtembelea na kutumia fursa hiyo kujadili majukumu ya msingi ya Ofisi yake ya kuratibu Shughuli za Serikali ikiwa ni pamoja na uratibu wa masuala ya maafa nchini ambalo ndilo eneo walilolenga kuzungumza na kuona namna bora ya kushirikiana na Serikali.
Mratibu wa Mpango wa Ulinzi wa Usalama na Utatuzi wa Mashambulizi (PSARP) - Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara Bw. John Spencer akizungumza jambo wakati wa kikao na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi walipomtembelea Ofisini kwake jijini Dodoma.

Kwa upande wake Mratibu wa Mpango wa Ulinzi wa Usalama na Utatuzi wa Mashambulizi (PSARP) - Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara Bw. John Spencer ameipongeza Serikali kwa namna inavyoendelea kutekeleza majukumu yake ikiwemo suala la menejimenti ya maafa huku akielea lengo la Mpango wa Ulinzi wa Usalama na Utatuzi wa Mashambulizi ambao umejikita katika kuimarisha utendaji wa polisi katika operesheni za dharura na kuona fursa katika kushirikiana na nchi ya Tanzania ili kuimarisha utendaji wa pamoja wa taasisi zinazohusika na kukabiliana na maafa.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (Katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na ujumbe kutoka Mpango wa Ulinzi wa Usalama na Utatuzi wa Mashambulizi (PSARP) wakiongozwa na Mratibu wa Mpango wa Ulinzi wa Usalama na Utatuzi wa Mashambulizi (PSARP) - Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara Bw. John Spencer (kushoto kwake)na kulia kwake ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya utafiti wa maafa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Charles Msangi.

Aliongezea kuwa wapo tayari kushirikiana ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuimarisha uwezo wa kukabiliana na maafa kwa kuwajengea uwezo wataalam wa maafa katika eneo la mfumo jumuishi wa utendaji wa pamoja wakati wa dharura.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news