DODOMA-Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoa wa Singida, sehemu ya mkoa wa Dodoma na sehemu ya mkoa wa Manyara utaanza tarehe 25 Septemba, 2024 hadi tarehe 01 Oktoba, 2024.
Wazee wa kimila ni wadau muhimu wa uchaguzi kutokana na umri, hekima na busara zao. Tume imekuwa ikishirikiana na wazee wa kimila katika kuwaelimisha na kuwashawishi wananchi kujitokeza na kushiriki kwenye michakato ya uchaguzi. Pichani ni Chifu wa Mkoa wa Singida, Mushenyi Senge Ndovu (kushoto) na Chifu wa Singida Vijijini, Kilongo Kika wakiwa katika mkutano wa wadau wa Uchaguzi kuhusu uboreshaji wa daftari la Kudumu la Wapiga Kura uliofanyika leo Septemba 13,2024 mkoani Singida.
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mstaafu, Mbarouk Salim Mbarouk ameyasema hayo leo tarehe 13 Septemba, 2024 jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi ikiwa ni maandalizi ya zoezi hilo.
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifungua Mkutano wa wadau wa uchaguzi Mkoani Dodoma leo Septemba 13, 2024.
“Mzunguko wa tano wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utajumuisha mkoa huu wa Dodoma katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Halmashauri za Wilaya ya Bahi, Chamwino na Kongwa, mkoa wa Manyara katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu na Wilaya ya Kiteto na Simanjoro na mkoa wa Singida ambapo uboreshaji utaanza tarehe 25 Septemba, 2024 hadi tarehe 01 Oktoba, 2024 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni,” amesema.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu Asina Omari akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa Wadau wa Uchaguzi Mkoani Singida leo Septemba 13, 2024 ambapo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imekutana na wadau mbalimbali wa uchaguzi kuwapa taarifa juu ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaotaraji kufanyika Mkoani humo kuanzia Septemba 25 hadi Okotoba mosi mwaka huu.
Amefafanua kuwa uboreshaji wa Daftari utahusu kuwaandikisha raia wa Tanzania waliotimiza umri wa miaka kumi na nane na zaidi au watakaotimiza umri huo wakati au kabla ya tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na ambao hawajapoteza sifa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi au sheria nyingine yeyote.
Katika hautua nyingine, akifungua mkutano wa wadau mkoani Singida, Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ambaye pia ni Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Asina Omari amesema kuwa Tume katika kuhakikisha kwamba inaenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia ikiwa ni pamoja na kurahisisha zoezi hili la uboreshaji wa Daftari, imeboresha mfumo wa uandikishaji ambao kwa mara ya kwanza utamuwezesha mpiga kura aliyepo kwenye Daftari kuanzisha mchakato wa kuboresha taarifa zake au kuhama kituo kwa kutumia aina zote za simu au kompyuta.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani akiwasilisha mada ya Uboreshaji wakati wa kufungua mkutano wa Wadau wa Uchaguzi Mkoani Singida leo Septemba 13, 2024 ambapo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imekutana na wadau mbalimbali wa uchaguzi kuwapa taarifa juu ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaotaraji kufanyika Mkoani humo kuanzia Septemba 25 hadi Okotoba mosi mwaka huu.
“Wanaotumia simu za kawaida (maarufu kama kitochi au kiswaswadu) nao wanaweza kutumia huduma hii kwa kupiga namba *152*00# na kisha watabonyeza namba 9 halafu wataendelea na hatua zingine kama itakavyokuwa inaelekezwa kwenye simu husika,” amesema.
Jaji. Asina amefafanua kuwa mtumiaji wa huduma hii, atatakiwa kufika kituo anachokusudia kujiandikisha ili akamilishe hatua za kupigwa picha, kuweka saini na kupatiwa kadi yake ya mpiga kura.
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Bw. Selemani Mtibora akiwasilisha mada kwa niaba ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, mada ya Uboreshaji wakati wa kufungua mkutano wa Wadau wa Uchaguzi Mkoani Dodoma leo Septemba 13, 2024 ambapo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imekutana na wadau mbalimbali wa uchaguzi kuwapa taarifa juu ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaotaraji kufanyika Mkoani humo kuanzia Septemba 25 hadi Okotoba mosi mwaka huu.
Wadau wa uchaguzi kutoka vyama vya Siasa, Makundi maalum ya Wanawake, vijana, watu wenye Ulemavu, Wazee wa Kimila, Wahariri wa vyombo vya Habari wakishiriki katika mkutano wa Tumen a Wadau wa uchaguzi uliofanyika leo Septemba 13, 2024 mkoani Dodoma.
Wadau wa uchaguzi kutoka vyama vya Siasa, Makundi maalum ya Wanawake, vijana, watu wenye Ulemavu, Wazee wa Kimila, Wahariri wa vyombo vya Habari wakishiriki katika mkutano wa Tumen a Wadau wa uchaguzi uliofanyika leo Septemba 13, 2024 mkoani Dodoma.
Wadau wa uchaguzi kutoka vyama vya Siasa, Makundi maalum ya Wanawake, vijana, watu wenye Ulemavu, Wazee wa Kimila, Wahariri wa vyombo vya Habari wakishiriki katika mkutano wa Tumen a Wadau wa uchaguzi uliofanyika leo Septemba 13, 2024 mkoani Singida.
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ulizinduliwa mkoani Kigoma tarehe 20 Julai, 2024 sambamba na kuanza kwa uboreshaji kwenye mikoa mitatu ya Kigoma, Tabora na Katavi na kufuatiwa na mikoa ya Geit, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu na Manyara katika Halmashauri za Wilaya ya Babati, Hanang, Mbulu na Mji wa Babati.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Tume awamu ya kwanza ya uboreshaji wa Daftari inatarajiwa kukamilika mwezi Machi, 2025.