DAR-Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zilizoanza kutumika kuanzia Jumatano, tarehe 4 Septemba, 2024 saa 6:01 usiku.
Kwa mujibu wa EWURA,wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa rejareja na jumla wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zilizoidhinishwa. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayekiuka AGIZO hili;