Fatman Scoop afariki akitumbuiza jukwaani

CONNECTICUT-Fatman Scoop (53) ambaye ni rapa maarufu nchini Marekani amefariki dunia baada ya kudondoka jukwaani.
Scoop alikuwa akitumbuiza mubashara usiku wa Ijumaa katika tamasha la bure la Green & Gold Party lililofanyika Hamden, Connecticut nchini Marekani.

Rapa huyo dakika za mwisho alionekana akiwachangamsha mashabiki jukwaani kwa kuwaambia wapige kelele na kuinua mikono juu ambapo ghafla alidondoka nyuma ya meza ya DJ.

Aidha, Scoop alikimbizwa hospitali ingawa alipofikishwa, madaktari walieleza kwamba tayari amefariki.

Scoop amewahi kufanya kolabo na wasanii kama Missy Elliott na Ciara mwaka 2005 kwenye ngoma ya Lose Control na baadaye na Mariah Carey kwenye ngoma ya It’s Like That.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news