Fundi umeme aliyehusika katika wizi wa mitandaoni hatiani kwa rushwa

DAR-Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni mkoani Dar es Salaam imemhukumu fundi umeme,Bw.Said Nasibu Kilanga adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja au kulipa faini ya shilingi 200,000.

Ni baada ya kukutwa na hatia katika kosa la kutoa rushwa kinyume na kifungu cha 15 (1) (b) & (2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 329 Rejeo la 2022.
Hukumu dhidi ya Bw. Said Nasibu Kilanga imetolewa hivi karibuni kutokana na shauri la jinai namba 218/2023 lililokuwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni mbele ya Hakimu Nabwike Mbaba.

Shauri ambalo liliendeshwa na Mwendesha Mashtaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Kinondoni,Bw. Aidan Samali.

Ilielezwa kuwa, mshtakiwa alifikishwa mahakamani hapo Septemba 5, 2023 kwa shtaka tajwa hapo juu ambapo mshtakiwa alitoa rushwa kiasi cha sh 50,000 kwa Askari Polisi wa Kituo cha Polisi Mburahati,Bw. Yusuph Nammohe.

Lengo ni ili amsaidie kumaliza tuhuma za wizi wa mtandaoni zilizokuwa zikimkabili kituoni hapo.

Mahakama katika hukumu yake imemkuta mshtakiwa na hatia na kumhukumu kifungo cha mwaka mmoja gerezani au kulipa faini ya shilingi 200,000 ambapo mshtakiwa amelipa faini hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news