Furaha ya wananchi Mbinga kwa Rais Dkt.Samia haipimiki

RUVUMA-Wananchi wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma kupitia kwa Naibu Waziri Nishati na Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa, Mhe.Judith Kapinga wamemshukuru Rais, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ya Umeme, Maji, Barabara, Shule za Sekondari na Msingi pamoja na Afya.
Pongezi hizo zimetolewa leo Septemba 25, 2024 wakati Mhe. Rais Samia akizindua jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Katika Sekta ya Nishati, Mfano wa miradi hiyo ni ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Mbinga chenye thamani ya shilingi bilioni 3 ambao utatekelezwa katika mradi wa kuboresha gridi ya Taifa Awamu ya Pili.
Aidha kwa upande wa umeme vijijini, katika Jimbo la Nyasa umeme umefika katika Vijiji vyote 84 kwa gharama ya shilingi Bilioni 83.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news