Gavana Tutuba atoa wito kwa IFC kuwekeza katika sekta binafsi nchini

DAR-Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba ametoa wito kwa Taasisi ya Fedha ya Kimataifa (International Finance Cooperation -IFC) kuwekeza katika sekta binafsi nchini kutokana na fursa mbalimbali zilizopo katika sekta hiyo.
Wito huo umetolewa na Gavana Tutuba, alipokutana na ujumbe wa IFC tarehe 10 Septemba, 2024 katika ofisi za Benki Kuu jijini, Dar es Salaam.

“Tumekuwa tukiwahimiza muwekeze kwenye sekta binafsi nchini kutokana na fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini,” amesema.

Aidha, ameueleza ujumbe huo kuwa tafiti ya Finscope ya mwaka 2023, zinaonesha kiwango cha utumiaji wa huduma rasmi za kifedha nchini kiliongezeka hadi kufikia asilimia 76% kwa mwaka 2023 na anaamini kiwango hicho kitaongezeka kutokana na jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali.
“Tumejiwekea shabaha kufikia 2028 kiwango cha utumiaji wa huduma rasmi za kifedha kifike asilimia 85% na uwezekano wa kufikia malengo hayo ni mkubwa kutokana na jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali ikiwemo usambazaji wa intaneti nchini kote kupitia mkongo wa Taifa ambao utarahisisha huduma za kifedha kwa njia ya mtandao nchini kote,” amesema.

Pia, ameongeza kuwa ili kukuza sekta ya biashara nchini serikali imefanya jitahada mbalimbali za kuzirasimisha kwa lengo la kuziwesha biashara hizo kwa lengo la kuzikuza na kupunguza uwepo wa biashara zisizo rasmi.
Naye, Mkurugenzi wa Taasisi ya IFC kwa Ukanda Afrika Mashariki, Bi. Mary Peschka, ameishukuru BoT kwa kuendelea kushirikiana na wadau wa sekta mbalimbali katika kusimamia uchumi wa nchi na ameahidi kuwa IFC itaendelea kushirikiana na Benki Kuu pamoja na serikali kiujumla kupitia uwekezaji katika sekta mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news