Hatujapata mbadala wa chama cha kuongoza nchi hii-Rais Dkt.Samia

NA GODFREY NNKO

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Ris wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema kuwa,mabadiliko makubwa yanayofanyika nchini ni kwa ajili ya kukiimarisha chama hicho na kwa sasa hakuna mbadala wa chama cha kuiongoza Tanzania.
Dkt.Samia ameyasema hayo leo Septemba 28,2024 wakati akifunga Kikao Maalum cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Taifa.

Ni katika ukumbi wa Parokia ya Bombambili katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

"Kwa wale wanaotaka twende tulivyozoea, mnaweza mkasikia malalamiko mengi, niwahakikishie ndugu zangu UWT mabadiliko yote yanayotokea ni kwa sababu ya kukiimarisha chama chetu, tukitambua kwamba bado hatujapata mbadala wa chama cha kuongoza nchi hii. Bado hatujakipata.

"Kwa hiyo, lazima tuimarike na kusimama imara kuendesha Tanzania ambayo tumeifungua kwa fursa nyingi sana, lazima tuimarike.

"Lakini, vile vile tumeshuhudia mabadiliko ndani ya chama chetu ya vitendea kazi, tumeweza kukipatia chama vitendea kazi na hakuna sababu kwa nini tushuke chini kwa asilimia 80 katika chaguzi zinazoendelea.

"Kwa sababu kata kuna vitendea kazi, wilaya kuna vitendea kazi, mkoa kuna vitendea kazi, Taifa kuna vitendea kazi na ndiyo maana mmesema mmeweza kuzunguka katika maeneo yote hayo kwa sababu mmewezeshwa kufanya hivyo.

"Hakuna sababu kwamba msiende kusimamia kazi ya chama ifanywe katika ngazi zote, lakini tunakiimarisha chama kwenye teknolojia pia, tunakwenda kukiimarisha chama kwenye teknolojia na ndiyo maana wamesema wamesajili hawa, waliopo kwenye mfumo hawa.

"Kwa hiyo, kazi ya kuwaweka wanachama kwenye mfumo inaendelea, ninataka niwape moyo kwmaba tumebeba suala la uchapishaji wa kadi na tayari kadi zinachapishwa, zitakuja kwa wingi,"amesisitiza Rais Dkt.Samia.

Hayo yanajiri ikiwa ni sehemu ya ziara ya Rais Dkt.Samia mkoani Ruvuma ambayo licha ya kuzungumza na wananchi ndani ya siku sita pia amezindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Katika hatua nyingine, Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) umelitaka Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) kumuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tansania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kumuita muuaji.

Mary Chatanda ambaye ni Mwenyekiti wa UWT Taifa amesema kuwa,"Tunawataka wanawake wa CHADEMA kuomba radhi na kuacha mara moja kukuita wewe muuaji.

"Tunawakumbusha wasishau walikualika kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Wanawake wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2023, kwa umuhimu wako walikupatia tuzo ya maridhiano ya kuwa Rais wa Kwanza Afrika na Duniani kukubali mwaliko kutoka chama cha upinzani."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news