RUVUMA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Septemba 27,2024 amezindua Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mchepuo wa Sayansi na Sanaa Namtumbo mkoani Ruvuma iliyopewa jina la ya Dr.Samia Suluhu Hassan ambayo ujenzi wake umegharimu shilingi bilioni 4.6.


Shule hii ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,200 na mpaka sasa wanafunzi waliopo ni 548.