PWANI-Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amelipongeza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kikosi cha Ruvu kwa juhudi za kuchangia maendeleo ya sekta ya uchumi.

Katika hotuba yake, Kunenge amesifu jeshi hilo kwa mchango wake katika jamii kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aidha, Kunenge aliomba Jeshi hilo kuendelea kuanzisha na kubuni miradi mipya, ikiwemo mradi wa bustani ya wanyamapori (Zoo) ambayo imekuwa kivutio kikubwa kwa watalii wa ndani na nje ya nchi.

Katika hatua nyingine, Kunenge ameshauri Jeshi hilo kushirikiana na taasisi kama TARURA ili kuboresha miundombinu ya barabara, jambo ambalo litachangia kuongeza mapato ya mkoa.
Kwa upande wake, Kamanda wa Kikosi cha 832 cha JKT Ruvu, Kanali Peter Elias Mnyani, amemshukuru kwa ushirikiano uliotolewa na taasisi mbalimbali mkoani Pwani wakati wa hatua za awali za vijana hao kujiunga na jeshi.

“Nimepata ushirikiano mkubwa kutoka RITA na NIDA katika hatua za awali za kujiunga kwa vijana,” amesema Kamanda Mnyani.