JKU FC yatembeza kichapo kwa Inter Zanzibar mabao 3-1

NA DIRAMAKINI

TIMU ya Inter Zanzibar imeambulia kichapo cha mabao 3-1 katika mechi ya kwanza ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Zanzibar (PBZ Premier League).
Kichapo hicho imetembezwa na JKU FC kupitia mtanange uliopigwa Septemba 6,2024 katika Dimba la New Amaan Complex jijini Zanzibar.

Bao la kwanza la JKU FC katika PBZ Premier League msimu wa 2024/25 limefungwa na Kofi Hamza dakika ya 7' ya kipindi cha kwanza.

Ni bao ambalo lilidumu dakika kadhaa ndipo Abdallah Hassan dakika ya 15 akasawazisha.

Katika kipindi cha dakika 45 za kwanza timu hizo mbili zilienda mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu ya sare ya bao 1-1.

Aidha, kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kutaka kupata ushindi, ingawa JKU FC iliwazidi ujanja Inter Zanzibar ambapo dakika ya 65, Neva Kaboma aliwapa raha mashabiki wa JKU FC.

Hata hivyo, Tariki Mohamed alifunga hesabu kwa kuiandikia JKU FC bao la tatu dakika ya 89 ya mtanange huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news