PERTH-Tanzania imetajwa kuwa nchi kinara kwa Bara la Afrika ambayo kampuni za Madini za Australia zimewekeza kwa asilimia 21% ya uwekezaji wote wa kwenye Sekta ya Madini.
Hayo yameelezwa leo Septemba 4,2024 mjini Perth, Australia wakati wa mkutano wa Africa DownUnder (ADU) unaowashirikisha wadau wa madini kutoka Australia na nchi za Bara la Afrika.


Waziri Mavunde amesema, utekelezaji wake utasaidia kuongeza mapato ya nchi,kuongeza nafasi za ajira,ushiriki wa watanzania (Local Content) na kuchochea ukuaji wa sekta ya madini.
Aidha,Waziri Mavunde alizitaka kampuni hizo kuheshimu mikataba waliyoingina na serikali na hasa katika kunufaisha watanzania kupitia wajibu kwa jamii (CSR).
Pia,utoaji huduma na usambazaji wa bidhaa migodini na ulipaji wa kodi na tozo stahiki ili rasilimali hizo zitoe mchango katika maendeleo ya uchumi wa nchi na watu wake.

Ni kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na hivyo kuvutia uwekezaji huu mkubwa nchini ambao utachochea kukuaji wa kasi wa uchumi wa Tanzania.