Magazeti leo Septemba 22,2024

KILIMANJARO-Serikali ipo katika hatua za mwisho kuanzisha Idara ya Ustawi wa Jamii inayojitegemea chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ili kurahisisha na kuimarisha uratibu, usimamizi na utekelezaji wa afua za Ustawi wa Jamii nchini.
Lengo la kuanzisha Idara ya Ustawi wa Jamii itakayojitegemea ni ongezeko la uhitaji wa huduma za Ustawi wa Jamii kisekta kunakohitaji taasisi madhubuti katika kusimamia na kuratibu utoaji wa huduma hizo katika jamii kupitia Taasisi za umma, binafsi na wananchi kwa ujumla.
Hatua hiyo ni matokeo ya kukubaliwa kwa wasilisho la mapendekezo ya Haki Jinai kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambapo mpango huo kwa sasa unasubiri maelekezo ya muundo wa Idara hiyo kupitia Wizara ya Utumishi.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima ameyasema hayo wakati akifunga mkutano wa tatu wa mwaka wa Maofisa Ustawi wa Jamii uliofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro.









Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news