Kocha Rachid Taoussi anaumiza kichwa Azam FC

NA DIRAMAKINI

SAFARI ya Azam FC katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara imeendelea kuwa na mapito, baada kushindwa kutamba kama kawaida yao.
Hayo yanajiri licha ya matajiri hao wa Chamazi, Azam FC kuachana rasmi na kocha Youssouph Dabo pamoja na benchi lake la ufundi.

Aidha,baadaye ilimtambulisha Rachid Taoussi ambaye ni raia wa Morocco kuwa kocha mkuu kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Rachid Taoussi alikuja na wasaidizi wake watatu ambao ni kocha msaidizi Ouajou Driss, kocha wa utimamu wa mwili Badr Eddine na kocha wa makipa Rachid El Mekkaoui.
Septemba 14, 2024 katika dimba lao la Azam Complex lililopo Kata ya Chamanzi, Kocha mkuu mpya, Rachid Taoussi ameanza kibarua chake.

Aidha, timu hiyo iliambulia sare tasa dhidi ya Pamba Jiji FC kutoka jijini Mwanza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news