Kuelekea Kongamano la Kihistoria la TEHAMA: Dkt.Mwasaga aeleza kwa nini Akili Mnemba (AI)

NA DIRAMAKINI

ZIKIWA ni siku za kuhesabika zimesalia kabla ya kufanyika Kongamano la Kihistoria la Teknolojiaya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) nchini ambalo limejikita zaidi katika Akili Mnemba (AI), Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA nchini (ICTC),Dkt. Nkundwe Moses Mwasaga amefafanua kwa kina kuhusu AI.

Amesema, Akili Mnemba ni mifumo ya kompyuta ambayo inasaidia kuifanya kompyuta kuwa na uwezo ambao unafananafanana na uwezo wa akili ya binadamu kwenye kufikiria na kufanya maamuzi.
Dkt.Mwasaga ameyasema hayp kupitia mahojiano mubashara na runinga ya ITV jijini Dar es Salaam katika kipindi cha Kumekucha.

Kwa ni ni akili memba? Dkt.Mwasaga anasema, "Kuna vitu vitatu ambavyo vimetokea duniani ambavyo vimewezesha akili mnemba sasa hivi iweze kufanya vitu ambavyo vinafanana na vya binadamu. Kumbuka akili mnemba ilianza siku nyingi ilianza karibu miaka ya 1950 huko.

"Lakini, wakati ule kuna vitu vitatu ambavyo havikuwepo kwa wakati mmoja, cha kwanza sasa hivi kuna taarifa nyingi (data), nyingi zinazalishwa kila siku kwenye mitandao ya kijamii na vitu vingine.

"Cha pili, sasa hivi tuna mifumo ya kompyuta ambayo yenyewe inaweza kuingia kwenye data na kutafuta taarifa ambazo zinaweza kusaidia katika kutoa maamuzi.

"Kitu cha tatu sasa hivi. uwezo wa kuchakata vitu umekuwa ni mkubwa na unapatikana tu kirahisi sana, ukiangalia simu zetu zina uwezo mkubwa sana wa kuweza kuchakata.

"Kwa hiyo kwa sasa hivi, hivyo vitu vitatu vyote vipo, na hivyo ndiyo vimesababisha sasa hivi mashine zinakuwa na uwezo wa kufikiria ambao upo katika hali fulani ambayo inafanana na binadamu, ingawa binadamu bado ana nafasi kubwa,"amefafanua Dkt.Mwasaga.

Ikumbukwe kuwa, kongamano hilo ni la kihistoria kwa sababu katika Bara la Afrika kwa mara ya kwanza kuna Shindano la Akili Mnemba na Roboti kwa vijana wote wa Afrika ambalo litazinduliwa kwa mara ya kwanza Tanzania.

Pia,litaenda sambamba na kongamano la TEHAMA la Taifa ambalo kwa mwaka huu kauli mbiu yake inasema kutumia Akili Mnemba na Roboti katika Kuleta Mapinduzi ya Kiuchumi na Kijamii.

Dkt.Mwasaga amesema, kongamano hilo linafanyika mwezi Oktoba kuanzia tarehe 13 hadi tarehe 17,2024.

"Na kongamano hili litakuwa la siku tano, kutakuwa kuna mambo mengi sana pale yanayohusiana na hiyo kauli mbiu na vile vile maonesho mbalimbali ya kampuni changa za startups za ndani ya nchi na nje ya nchi. KWA KINA TAZAMA MAHOJIANO HAPA CHINI:

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news