Kwa umoja wetu tukemee maovu katika jamii- Alhaj Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezishauri taasisi za dini kushirikiana na taasisi za Serikali na binafsi kukemea maovu yote ndani ya jamii.
Rais Alhaj Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo Septemba 18,2024 alipozungumza katika Baraza la Maulid Ukumbi wa Idrissa Abdul Wakil Kikwajuni, Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa,  suala hilo sio la kuachiwa taasisi au mtu mmoja bali ni wajibu kushirikiana kukabiliana na maovu hayo kwa pamoja.
Rais Dkt.Mwinyi amewasisitiza wananchi kuendelea kushikamana na na kupendana kuepuka mifarakano ili kujenga nchi na kuleta maendeleo ya haraka.
Halikadhalika Alhaj Dkt.Mwinyi akizungumzia suala la maadili ya usomwaji wa Maulid amelishauri Baraza la Maulidi kwa kushirikiana na Afisi ya Muft kutoa maelekezo na miongozo kupitia wanazuoni wa ndani na nje ya nchi kurejesha misingi sahihi ya kimaadili.
Kwa upande mwingine Rais Alhaj Dkt.Mwinyi amewaasa Waislamu kufuata maelekezo na mafunzo ya Mtume Muhammad (SAW) Ili kudumisha Amani ikiwemo kupendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news