DODOMA-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Mhe. Ridhiwani Kikwete amepongeza Baraza la Ushauri wa Masuala ya Kazi, Uchumi na Kijamii (LESCO) kwa utekelezaji mzuri wa majukumu yake.
Mhe. Ridhiwani ametoa pongezi hizo leo Septemba 5, 2024 jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa Baraza hilo wanaomaliza muda wao.


Aidha, amesema katika kipindi cha miaka mitatu, LESCO imefanya kazi nzuri ya kuishauri serikali kuhusu sera zinazohusu masuala ya Ajira na Kazi; upangaji wa kima cha chini cha mshahara katika sekta binafsi; Uridhiaji wa mikataba ya Shirika la Kazi Duniani; na ushirikishwaji wa wadau wa Utatu (Serikali, Waajiri na Wafanyakazi) katika masuala ya kazi, Uchumi na jamii.

Tags
Habari
LESCO Tanzania
Ridhiwani Jakaya Mrisho Kikwete
Ridhiwani Kikwete
Waajiri Tanzania
Waajiriwa Tanzania
Wizara ya Kazi na Ajira