Ligi Kuu ya Zanzibar (PBZ Premier League) yazidi kunoga

NA DIRAMAKINI

LIGI Kuu ya Zanzibar (PBZ Premier League) imeendelea kutimua vumbi leo Septemba 8,2024 huku ushindani ukionekana kuwa mkubwa.

Septemba 7,2024 ilipigwa michezo miwili ambayo ilizikutanisha Mlandege FC dhidi ya Chipukizi, wakati Mwenge walikuwa dhidi ya KVZ FC.

Kupitia mtanage wa Mlandege dhidi ya Chipukizi ambao ulipingwa katika dimba la New Amaan Complex jijini Zanzibar, miamba hiyo ilitoka sare ya bila kufungana.

Mechi ya pili ya Mwenge dhidi ya KVZ FC ilikuwa ya kicheko kwa KVZ baada ya Samson Kwakwala dakika ya 44 kupachika bao safi

Ni katika dimba la Gombani lililopo Kisiwani Pemba, hivyo hadi dakika 90 zinatamatika KVZ FC walizoa alama tatu kupitia bao 1-0.
Aidha, leo Septemba 8,2024 katika dimba la New Amaan Complex bao pekee la Robert Pius dakika ya 57 limetosha kuipa alama tatu,Muembe Makumbi.

Kupitia mtanange huo, Muembe Makumbi walichuana na New City. Vilevile katika dimba la Gombani lililopo Kisiwani Pemba,Tekeleza wamejikuta katika wakati mgumu.

Ni baada ya Kipanga kuwagonga mabao mawili kwa sufuri, bao la kwanza liliwekwa nyavuni na Suleiman Hussein dakika ya 59 huku bao la pili likifungwa na Kombo Ramadhan (Og) dakika ya 85.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news