Lindeni misitu na kuitunza, si kuichoma-Rais Dkt.Samia

RUVUMA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi kuacha tabia ya kuchoma misitu bali wailinde na kuihifadhi.
Ameyasema hayo leo Septemba 26, 2024 katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara.
“Tatizo jingine ndugu zangu ninalotaka kuwaambia ni uchomaji wa moto. Jamaa zangu mmezidi kuchoma moto. Mkichoma moto mnaharibu misitu.

"Mkichoma moto mpaka pembeni kwa barabara humo ukipita moto unawaka. Lami ile ikipata moto inayeyuka barabara zinaharibika.

"Acheni kuchoma misitu moto, na kama ni lazima uchome moto shamba linda moto usitapakae kwenda kuharibu maeneo mengine ya misitu yaliyohifadhiwa."
Amesema, wananchi wanapochoma misitu moto inaharibu misitu pamoja na miundombinu ya barabara hivyo inarudisha nyuma maendeleo.

Kuhusu changamoto ya tembo iliyowasilishwa na Mbunge wa Jimbo la Namtumbo, Mhe. Vita Kawawa, Rais Samia amesema changamoto hiyo inaendelea kupatiwa ufumbuzi na Wizara ya Maliasili na Utalii chini ya Waziri Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news