Kwa mujibu wa Kifungu vya 11 (2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, Tume inatakiwa kuweka wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura ili kutoa fursa kwa wananchi:
- Kulikagua Daftari;
- Kufanya marekebisho ya majina au mahali wanapoishi;
- Kuingiza au kufuta majina ya Wapiga Kura;
- Kuweka pingamizi kwa Mpiga Kura aliyeandikishwa na hana sifa za kuwemo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Kumuwekea Pingamizi aliyeandikishwa kwenye Daftari la Awali
Kifungu cha 27 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024,kinaruhusu Mkurugenzi wa Uchaguzi au Afisa Mwandikishaji au mtu yeyote aliyeandikishwa kuwa Mpiga Kura, kuweka pingamizi dhidi ya jina lililopo katika Daftari la Awali la Wapiga Kura. Soma kwa kina hapa》》》
Tags
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
Habari
INEC Tanzania
Kuelekea Uchaguzi
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi