Maadhimisho ya Siku ya Viziwi yaanza rasmi mkoani Shinyanga

SHINYANGA-Maadhimisho ya Wiki ya Viziwi Kitaifa yamezinduliwa rasmi Septemba 25, 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi ambapo maadhimisho hayo yanaongozwa na Kauli Mbiu isemayo "Ungana Kutetea Haki za Lugha ya Alama."
Akizungumza wakati wa ufunguzi, Mhe. Macha ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu na Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) kwa ushirikiano mzuri ambao umekuwa na tija katika kukuza ustawi wa Watu wenye Ulemavu ikiwemo Viziwi.

"Serikali inatambua umuhimu wa kuwekeza katika lugha ya alama na ndio maana mpaka sasa vipo Vyuo vya Serikali na Taasisi binafsi zinazotoa mafunzo ya lugha ya alama," asemema.Aidha, ametoa rai kwa Wizara yenye dhamana ya Watu wenye Ulemavu, Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) na wadau mbalimbali kuendelea kutoa elimu mbalimbali kwa Viziwi pamoja na Watu wenye Ulemavu.

Naye Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Gerold Komba amesema serikili imeendelea kuhakikisha watoa huduma katika Taasisi mbalimbali wanajengewa uwezo ili wapate elimu ya awali ya lugha ya alama ili kuweza kuhudumia kundi hilo.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA), Bi. Selina Mlemba, amesema maadhimisho ya wiki ya Viziwi Kitaifa ambayo yanaadhimishwa Mkoa Shinyanga yataambana na makongamano ambayo yanalenga kukuza uelewa kwa taasisi na jamii katika kushirikisha watu Wenye Ulemavu.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete anatarajiwa kiwa mgeni rasmi katika Kilele cha Wiki ya Viziwi tarehe 28 Septemba, 2024, mkoani Shinyanga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news