MOROGORO-Maafisa wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) wanapata mafunzo maalum ya kimataifa juu ya utoaji wa elimu kuhusu matumizi ya dawa za kulevya.

Hii ni sehemu ya mikakati ya Mamlaka ya kuzuia matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya kupitia elimu sahihi kwa jamii.