Maendeleo ni makubwa nchini,Watanzania tumuunge mkono Rais Dkt.Samia-Mathias Canal

SINGIDA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan anapaswa kutiwa moyo na kuungwa mkono kwa maendeleo makubwa anayoyafanya kwa ajili ya watanzania sio kubezwa au kumkejeli.Wakati Tanzania inapata Uhuru mwaka 1961 ilikuwa na Chuo Kikuu kimoja ila kwa sasa ameipaisha sekta ya elimu na kuwa na vyuo vikuu 30 na vyuo vishiriki 12 mpaka sasa.

Kwenye Wilaya ya Iramba kulikuwa na shule nne za msingi na sasa zipo za msingi 111 ambapo za serikali ni 108 na shule binafsi ni 3, kwa upande wa shule ya sekondari Wilaya ya Iramba likuwa na shule 1 na sasa zipo 29 ambapo za Serikali ni 26 na za binafsi zipo tatu.
Hayo yamebainishwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa WazoHuru Media Group Ltd,ndugu Mathias Canal, tarehe 19 Septemba 2024 ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 61 ya Shule ya Msingi Kiomboi-Bomani iliyopo wilayani Iramba katika Mkoa wa Singida na kuongeza kuwa Rais Dkt.Samia ni mwanasiasa mstahimilivu na mwenye utulivu wa hali ya juu katika uongozi wake.

Mathias ameeleza kuwa,mwaka 2022 Serikali ilifanya mapitio na mabadiliko ya mitaala na Sera ya Elimu ya mwaka 2014 hatimaye kuwa na toleo jipya la sera ya elimu ya mwaka 2023.
Amesema, kwa ujumla katika sera hiyo ya elimu kutakuwa na mambo muhimu ikiwemo Kutoa elimu ujuzi badala ya taaluma pekee, na Elimu ya lazima itakuwa miaka 10 badala ya 7.

Mathias Canal amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof Adolf Mkenda kwa kuja na wazo la ujenzi wa vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) ambapo Wilaya ya Iramba imepokea Bilioni 1.4 na ujenzi wa VETA unaendelea katika Kijiji cha Salala Kata ya Old Kiomboi.

Hali kadhalika amempongeza Mbunge wa Jimbo la Iramba ambaye ni Waziri wa Fedha, Mhe.Dkt.Mwigulu Mchemba kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali nchini ikiwemo katika jimbo lake ambapo katika kipindi cha miaka minne 2020-2024 Wilaya ya Iramba imepokea Bilioni 6.682 kwa ajili ya sekta ya elimu.
Katika mahafali hayo ndugu Mathias Canal amechangia kiasi cha Shilingi 400,000 kwa ajili ya motisha kwa walimu, Mipira 6 na jezi jozi mbili. Mipira mitatu na jezi jozi moja kwa ajili ya mchezo wa mpira wa miguu (Football) na mipira mitatu na jezi jozi moja kwa ajili ya mchezo wa mpira wa pete (netball).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news