Mafanikio yaliyopo Sekta ya Kilimo hayatokei kwa bahati mbaya-Rais Dkt.Samia

RUVUMA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema, mafanikio yaliyopo sekta ya kilimo hayatokei kwa bahati mbaya bali ni kutokana na juhudi uwekezaji mkubwa uliofaywa na Serikali.
Amesema, zao la kahawa pekee limeongezeka katika uzalishaji kutoka tani 65,000 hadi kufikia tani 85,000,hivyo kuingiza dola milioni 250 nchini.

Ameitaka Wizara ya Kilimo kuhakikisha wawekezaji waliopo mbali wanayoyafanya katika kurudisha kwa jamii za wanahusisha kurithisha ujuzi na teknolojia hususami za umwagiliaji zinazotumika katika sekta hiyo ili kuwezesha wananchi kuwa na kilimo chenye tija kwa maslahi ya vizazi vijavyo.

Rais Dkt.Samia amesema hayo leo Septemba 24,2024 alipotembelea shamba la uzalishaji wa Kahawa la AVIV mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa maghala 28 ya kuhifadhi mazao ya nafaka yaliyo chini ya Wakala wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wilayani Songea mkoani Ruvuma katika muendelezo wa ziara yake ya siku sita mkoani huko.

Pia,Rais Dkt.Samia ametaka wakulima watumie fursa ya kupanda kwa bei ya kahawa, kuhifadhi fedha ili wasitaabike kipindi bei itakaposhuka

“Misimu ikiwa mizuri na bei ikiwa nzuri tuwe na mifumo ya kujiwekea akiba ili mabadiliko ya tabianchi yanapotokea tuwe na akiba,” amesema.

Ameitaka Wizara ya Kilimo kujipanga vyema na masharti yanayotolewa na masoko ya kimataifa ya kahawa hasa lile la uzalishaji bila kukata misitu.

Pamoja na kutokata misitu, amesema masharti mengine ni kukagua, kuyasajili na kupeleka taarifa za mashamba kwenye masoko hayo ili ijulikane linakotoka zao husika.

“Wanatambua tusikate misitu,kule kwao wameshakata, lakini sisi tunataka soko, tunapaswa kuhakikisha tunayatimiza masharti ili kupata soko,” amesema.
Pia ameagiza wizara kufanya uchunguzi wa madai ya wakulima wa kahawa kukatwa fedha kinyemela na vyama vikuu vya ushirika.

Amesema, anatambua kuwepo kwa malalamiko hayo yaliyosababishwa na ongezeko la bei ya kahawa mwaka huu.

“Ninatambua uwepo wa malalamiko ya wananchi kwamba kwa sababu kahawa imepanda bei, baadhi ya vyama vikuu vya ushirika (hakuvitaja) vinawakata wakulima kinyemela,” amesema.

Amemtaka Waziri Bashe afuatilie ili kuwa na mfumo wa wazi utakaowafanya wakulima kuona wanachouza na uhalisia wa makato yao.

“Huu ujanja ujanja unaoendelea unapaswa kukomeshwa,”amesema Rais Dkt.Samia alipotembelea shamba hilo lenye ukubwa wa hekta 200.
Hata hivyo, amesema ongezeko la bei hiyo na malipo ya haraka kwa wakulima wa kahawa ni matokeo ya juhudi za Serikali za kuongeza ufanisi katika mauzo ya zao hilo.

Katika hatua nyingine, Rais Dkt.Samia ameutaka uongozi wa shamba hilo,kufanya shughuli za kijamii,ujikite katika uchimbaji wa visima vya umwagiliaji kwenye mashamba ya wakulima.

Amesema,kufanya hivyo, kutawawezesha wakulima kuzalisha kahawa kwa umwagiliaji na kuuza kwa Aviv.

Awali, akizungumza katika ziara hiyo, Waziri Hussein amesema, shamba hilo ni moja kati ya mashamba 50 yanayozalisha kahawa na kwamba hilo ni kubwa zaidi ya mengine yote.

Amesema, asilimia 60 ya kahawa inayozalishwa na shamba hilo inauzwa nje ya nchi kwa Kampuni ya Strabag.

Hata hivyo, amesema wastani wa bei ya kahawa mwaka huu ni Dola 4.3 za Marekani, kiwango ambacho ni tofauti na nyakati zilizopita.

Amesema,mafanikio yaliyopo sekta ya kilimo yametokana na maamuzi ya kisera na sheria ya Rais Dkt.Samia hususani katika kuboresha sekta ya uwekezaji na kurudisha masoko.
“Hali hii imerudisha uhai wa uzalishaji kwa wawekezaji na wakulima wa ndani,shamba hili linategemea zaidi shughuli za umwagiliaji hivyo wizara tumemuagiza mwekezaji uchimbaji wa visima na mabwawa unufaishe jamii katika mashamba ya wananchi,”amesema

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama ameishukuru serikali kwa maamuzi ya kisera yanayovutia uwekezaji na kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali.

Mhagama ambaye pia ni Waziri wa Afya ameeleza kuwa,mradi wa AVIV umekuwa na faida nyingi kwa jamii, na mwekezaji ameshirikiana na uongozi wa serikali kuandaa mpango wa urithishaji wa mchakato wa kilimo cha kahawa.

Aidha,mwekezaji huyo pia anachangia hadi bilioni 1 kwa Halmashauri ya Wilaya Peramiho mkoani Ruvuma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news