Mafunzo ya Clinical Phamacy Services yafunguliwa Bugando

MWANZA-Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, Sr. Dkt. Alicia Massenga akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Bugando, amefungua rasmi mafunzo ya Huduma tabibu za kifamasia (Clinical Phamacy Services) yanayotolewa kwa Wafamasia kutoka kanda mbalimbali nchini kuanzia terehe 17 mpaka tarehe 27 Septemba, 2024 katika Hospitali ya Bugando.
Mafunzo hayo yanaendeshwa na Chuo Kikuu cha Sayansi Shirikishi (MUHAS) kwa udhamini wa shirika la Christian Social Services Commission (CSSC) yakiwa na jumla ya Wafamasia 30 kutoka hospitali mbalimbali nchini.

Sr.Dkt Massenga amewapongeza waandaaji na washiriki na kuwataka kutumia vizuri mafunzo hayo kwani yana tija kubwa katika kumhudumia mgonjwa.

"Niwapongeza CSSC kwa mafunzo haya yenye matunda makubwa ambayo kwa kweli tumekuwa tukiyaona katika kuboresha Sekta ya Afya.

"Washiriki tutumie muda mwingi kwenye mafunzo haya, mzingatie yote mtakayopata hapa na mkayatumie huko muendako kumhudumia mgonjwa na kuwafundisha wengine kwa kufanya kazi kwa umoja.

"Mkifanya hivyo itaongeza ufanisi kwani itasaidia Mgonjwa kutumia dawa kwa wakati na itapunguza gharama za matibabu, mkatumie ujuzi huu vyema," ameyasema hayo Sr. Dkt Alicia Massenga.

Kwa upande wake Dkt. Andrew Charles ambaye ni meneja wa CSSC Kanda ya Ziwa amesema, mafunzo hayo ni muhimu kwani wafamasia watashirikiana na Madaktari moja kwa moja katika kumhudimia Mgonjwa.

Mafunzo ya Huduma tabibu za kifamasia (Clinical Phamacy Services) yanaendeshwa kwa siku 10 kwa washiriki 30 kutoka Mikoa ya Kilimanjaro, Tabora, Simiyu, Kigoma, Shinyanga, Mwanza na Mara kushiriki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news