Magazeti leo Septemba 11,2024

TANGA-Familia ya Mjumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),marehemu Ali Mohamed Kibao aliyezikwa Septemba 9,2024 jijini Tanga imeiomba Serikali kuharakisha uchunguzi wa kifo cha baba yao ambaye mwili wake ulipatikana maeneo ya Ununio jijini Dar es Salaam akiwa ameuawa. Ni baada ya kutekwa na watu wasiojulikana Septemba 6, 2024 katika maeneo ya Tegeta karibu na Jengo la Kibo Complex akiwa katika basi la Tashrif akielekea jijini Tanga.
Ombi hilo wamelitoa Septemba 10,2024 mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya Waziri huyo kufika nyumbani kwa marehemu jijini Tanga kutoa salamu za pole kwa niaba ya Serikali ambapo pia aliwasilisha rambirambi ya shilingi milioni 5.

Mtoto wa marehemu Mzee Kibao, Mariam Ali Mohamed ameiomba,Serikali kufanya uchunguzi wa kifo cha Baba yao huku akiomba familia iwe inapatiwa taarifa za uchunguzi huo na isipite muda mrefu bila matokeo ya uchunguzi kutoka huku akiomba majibu ya uchunguzi yawafikie familia kwa njia rasmi na sio kusikia kupitia vyombo vya habari.






Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news