Magazeti leo Septemba 14,2024

KILIMANJARO-Jeshi la Polisi nchini limepiga marufuku maandamano ambayo yametangazwa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe yanayotarajiwa kufanyika kuanzia Septemba 23, 2024 jijini Dar es Salaam.

Mbowe alitangaza maandamano hayo, kwenye makao makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yaliyopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam wakati akitoa msimamo wa chama hicho kufuatia matukio ya utekaji yanayoendelea nchini.
Mwenyekiti huyo wa CHADEMA alisema, iwapo Serikali haitawarudisha viongozi wao waliotekwa, sambamba na kuwatangaza wahusika wa vitendo hivyo vya utekaji, wataandamana kuanzia Septemba 23, 2024.

Akitangaza kupiga marufuku maandamano hayo Septemba 13, 2024 mkoani Kilimanjaro, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, SACP David Misime alisema, anashangazwa na kitendo cha viongozi wa chama hicho kuitisha maandamano wakati uchunguzi wa matukio hayo unaendelea.

Aidha, tayari Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameliagiza jeshi hilo na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kufuatilia na kuwasilisha taarifa kwake.















Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news