Magazeti leo Septemba 21,2024

DODOMA-Wananchi wa Kijiji cha Ngomai kilichopo Kata ya Ngomai katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma wamempongeza Mganga wa Zahanati ya kijiji, Dkt.Peter Mwakalosi kwa kumnunulia kiwanja huku akitarajiwa kujengewa nyumba kwa kuridhishwa na huduma za afya ambazo wamekuwa wakipatiwa na mtumishi huyo.
Wananchi hao kupitia hotuba iliyosomwa na Mtendaji wa Kijiji, Michael Mwisho wamesema, wamemnunulia mganga huyo kiwanja na wanatarajia kumjengea nyumba kama shukrani kutokana na kujitoa kwake kuisaidia jamii hiyo iliyokua na changamoto kwenye masuala ya huduma za afya.

“Tumeonesha nia na upendo wetu kwa Dkt. Mwakalosi hivyo, tulimchangia jumla ya shilingi Milioni 4 na elfu 16 ndipo jamii ilikubaliana inunue uwanja ili kumkabidhi Dr. Mwakalosi kiwe kiwanja chake binafsi na kilinunuliwa kwa fedha kiasi cha shilingi Milioni 3.6."








Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news