Mahakama ya Tanzania yashtuka, yazuia mahakimu kuhamia taasisi nyingine


MAGRETH KINABO,
INNOCENT KASHA
Mahakama

MWENYEKITI wa Tume ya Utumishi ya Mahakama, ambaye pia ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ametoa msimamo wa Tume kuwa haitawachia Mahakimu wake kwenda kufanya kazi mahali pengine, kwa sababu tayari Mahakama imeshawajenga na kuwapika ili waweze kutoa huduma ya utoaji haki kwa ubora na ufanisi.
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Mahakama, ambaye pia ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akimwapisha Hakimu Mkazi Mpya Mhe. James Kapele wakati wa hafla ya uapisho wa Mahakimu wakazi 22 ulifanyika jijini Dar es Salaam.

Aidha, Mwenyekiti huyo, amewataka watu wengine wanaowahitaji Mahakimu hao, kuiga mfano wa Mahakama ya Tanzania wa kuwaajiri wanasheria wengine wasio na ajira, na kuwajengea uwezo na kuwapika.

Uamuzi huo umetolewa leo tarehe 20 Septemba, 2024 na Mwenyekiti, huyo wakati akitoa hotuba yake mara baada ya kuwaapisha Mahakimu Wakazi wapya 22 wa Mahakama za Mwanzo, kwenye hafla iliyofanyika katika Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia (IJC),kilichopo Temeke jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Mahakama, ambaye pia ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa hutoba mbele ya Mahakimu Wakazi Wapya 22 (hawapo pichani) walioapishwa leo tarehe 20 Septemba, 2024 katika Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia -Temeke jijini Dar es Salaam.

“Kwa hiyo sisi tunapowachukua hatuna nia ya kuwaachia. Watakuja watu wengine wenye mishahara zaidi watasema tunataka hakimu fulani, hatuwapi tunawambia wao wawe na mipango ya kuwa na wanasheria ambao wapo wengi, ambao hawana ajira na wanasubiri ajira wawachukue na kuwapa mafunzo na kuwatengeneza wakawe wenyeviti wa mabaraza ya ardhi.

“Kwa hiyo tuelewane tunawachukua hatuna talaka, sisi hatuachani na ninyi, Huu ndio msimamo wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kuwa haitawachia wafanyakazi bora,” amesema Mhe. Prof. Juma.
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Mahakama, ambaye pia ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitia saini hati ya kiapo cha Hakimu Mkazi mara baada ya kumuapisha.

Mwenyekiti huyo, alisema Mahakama iko tayari kutoa mafunzo kwa wanasheria hao, watakaoajira na watu wengine kupitia Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto(IJA) au kusaidia kuwafundisha kupitia Majaji au Mahakimu wenye uzoefu.

Mhe. Prof. Juma alisema mfumo wa ajira wa Mahakama ni wa kujitahidi kuwajenga mahakimu ili waweze kutoa huduma bora zaidi.

“Sisi tunawajenga kimaadili na kiuwezo na ndio maana mchakato wa kuwapata Mahakimu unachukua muda mrefu,”amesisitiza Mwenyekiti huyo.
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Mahakama, ambaye pia ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akimwapisha Hakimu Mkazi Mpya Mhe. Lilian James Kombe wakati wa hafla ya uapisho wa Mahakimu wakazi 22 ulifanyika jijini Dar es salaam.

Akizungumzia kuhusu uendeshaji na usimamizi wa shughuli za kimahakama, alisema majukumu ya Mahakimu hao yameainishwa kwenye Katiba, Sheria na Kanuni mbalimbali. Ibara ya 107A (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano (1977) inawaelekeza Mahakimu na Majaji kufanya maamuzi ya mashauri ya madai na jinai kwa kuzingatia sheria.

Hivyo Ibara hiyo inakwenda mbali zaidi kwa kuwataka kuzingatia pia misingi kadhaa za utoaji haki,ambayo ni kutenda haki kwa wote bila ya kujali hali ya mtu kijamii au kiuchumi. Pili kutochelewesha haki bila sababu ya kimsingi. Tatu, kuamuru fidia ipasayo kwa watu wanaoathirika kutokana na makosa ya watu wengine, na kwa mujibu wa sheria mahsusi iliotungwa na Bunge.
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Mahakama, ambaye pia ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitia saini hati ya kiapo cha Hakimu Mkazi Mhe. Kuruthum Said Mkundawatu mara baada ya kumuapisha.

Nne kukuza na kuendeleza usuluhishi baina ya wanaohusika katika migogoro. Tano, kutenda haki bila kufungwa kupita kiasi na masharti ya kiufundi yanayoweza kukwamisha haki kutendeka.

Hata hivyo, aliongeza kwamba kazi ya Jaji au Hakimu ni huduma kwa binadamu. Maamuzi, hukumu na amri zenu Mahakimu ni lazima:

ziwe zinaeleweka, zinatekelezeka, zinatatua migogoro na zinajibu hoja zilizoletwa mahakamani.Upande utakaoshinda lazima ufahamu sababu za kushinda, na upande utakaoshindwa upewe sababu kwa nini umeshindwa.
Sehemu ya Mahakimu Wakazi wapya 22 wa Mahakama za Mwanzo wakifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Mahakama, ambaye pia ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (hayupo pichani), kwenye hafla iliyofanyika katika Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia (IJC),kilichopo Temeke jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Mahakimu Wakazi wapya 22 wa Mahakama za Mwanzo wakifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Mahakama, ambaye pia ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (hayupo pichani), kwenye hafla iliyofanyika katika Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia (IJC),kilichopo Temeke jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya jopo la Viongozi waandamizi wa Mahakama ya Tanzania likiongozwa na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani (wa kwanza kulia) wakifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Mahakama, ambaye pia ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (hayupo pichani), kwenye hafla iliyofanyika katika Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia (IJC),kilichopo Temeke jijini Dar es Salaam.

Akielezea kuhusu uzito wa kiapo cha Hakimu, alisema kinakukumbusha wajibu mzito uliopewa naJamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Kazi ya Uhakimu. Hivyo kiapo cha Uhakimu ni sehemu ya Utumishi wao kwani kinawakumbusha kuwa wanatakiwa kufanya kazi kwa uaminifu mkubwa, bila upendeleo wowote na kwa kuzingatia Katiba, Sheria na Kanuni za Maadili za Maafisa Mahakama.
"Mahakimu jihadharini kukiuka Maadili kwa kujihusisha na kutoa ushauri kuhusu mashauri yaliyo mbele ya Mahakimu Wenzenu. Jihadharini na ndugu, jamaa, marafiki wenye mashauri mahakamani ambao watawatembelea nyumbani kuwasimulia lakini kwa lengo la kupata ushauri au kukuvuta uwakosoe Mahakimu wenzako kuhusu shauri linaloendelea Mahakamani,” amesema.

Halikadhalika Mwenyekiti huyo, aliwaasa Mahakimu hao kufahamu kuwa miongozo ya MahakamaKuu na Mahakama ya Rufani imerahisishwa na urahisi wa kuzisoma hukumu zinazopandishwa katika mfumo wa TANZLII. Hivyo hakuna sababu ya kukosea kwenye maamuzi kwani miongozi inapatikana kwa urahisi.
Meza Kuu ikiongozwa na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Mahakama, ambaye pia ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mahakimu Wakazi wapya mara baada ya hafla ya uapisho.
Meza Kuu ikiongozwa na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Mahakama, ambaye pia ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mahakimu Wakazi wapya mara baada ya hafla ya uapisho.
Meza Kuu ikiongozwa na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Mahakama, ambaye pia ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mahakimu Wakazi wapya mara baada ya hafla ya uapisho.

Kwa sasa hata kama huna mtandao unaweza kupata maamuzi ya TANZLII kupitia mpango wa Sheria Mfukoni (POCKET LAW) ambao unakuwezesha kupata maamuzi ya TANZLII hata ukiwa huna mtandao.

Wakizungumza kwa niaba ya wengine, Mahakimu James Kapele na Kuruthumu Said Mkundawatu, wamesema wanashukuru kufikia hatua hiyo na kuahidi kutoa haki kwa wananchi kwa wakati.
Meza Kuu ikiongozwa na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Mahakama, ambaye pia ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waandamizi wa Mahakama ya Tanzania mara baada ya uapisho wa Mahakimu Wakazi 22 Temeke jijini Dar es salaam.
Meza Kuu ikiongozwa na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Mahakama, ambaye pia ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wanachama wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA).(Picha na Innocent Kansha- Mahakama).

Mahakimu hao watapatiwa mafunzo elekezi kuanzia Septemba 23, 2024 hadi Oktoba, 2024. Lengo mafunzo hayo ni kuwawezesha Mahakimu wapya kuielewa Mahakama pamoja na utamaduni wake na misingi yake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news