ZANZIBAR-Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hemed Seleima Abdulla amefungua Mkutano wa tatu wa kimataifa wa Tume ya Kupambana na dawa za kulevya kwa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESACD) jana tarehe tarehe 3 Septemba, 2024, katika hotel ya Verde visiwani Zanzibar.Mhe. Abdulla ameeleza kuwa, matunda ya mkutano huo yataongeza chachu katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya hasa katika kudhibiti wafanyabiashara, watumiaji wa dawa za kulevya pamoja na kuwasaidia walioathiriwa na matumizi ya dawa hizo.
Mkutano huu unalenga kujadili tatizo la dawa za kulevya, na kuweka mikakati yenye lengo la kutumia njia za kisayansi kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya hususani katika kupunguza madhara yatokananyo na matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa nchi wananchama wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Kimataifa
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)