Mama Mariam Mwinyi ashiriki mkutano wa Rockerfeller Foundation



NEW YORK-Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mhe. Mama Mariam Mwinyi ameshiriki katika mkutano ulioandaliwa na Rockerfeller Foundation.Lengo la mkutano huo ambao umefanyika Septemba 23,2024 City University of New York, Marekani lilikuwa ni kujadili lishe bora kwa watoto wa elimu ya awali.

Pia,mkutano huo umejikita kujadili uwekezaji katika mlo bora na kuandaliwa katika mazingira bora ikiwemo kuzingatia nishati safi.
Bi.Elizabeth Yee, Makamu wa Rais wa Programu, Rockerfeller Foundation alisema, wanahitaji takribani shillingi 170,000 tu kumlisha mtoto mmoja kwa mwaka mzima.
"Lakini, wakati huo huo tukumbuke kuwa milioni 7.5 ya tani za kuni hutumika katika kuandaa chakula cha watoto mashuleni chini ya Jangwa la Sahara, Afrika."
Mama Mariam amesema, ni muhimu kujifunza kwa wengine na kuhakikisha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na wadau wanashirikiana kuandaa rasilimali watu bora, watakaolijenga taifa letu baadae kwa kuwapa lishe bora wakiwa mashuleni bila kuathiri mazingira.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news