Mama Mariam Mwinyi ateta na uongozi wa Wakfu wa Ford jijini New York

NEW YORK-Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF),Mhe. Mama Mariam Mwinyi amekutana na uongozi wa Ford Foundation wakiongozwa na Bi. Monica Aleman, Mkurugenzi wa Programu za Kimataifa.
Ni Septemba 25,2024 katika ofisi za Ford Foundation jijini New York, Marekani.

Katika mazungumzo hayo, Mhe. Mama Mariam alieleza changamoto kubwa zilizopo kwenye masuala ya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia ikiwa pamoja na juhudi za Serikali za kuanzisha Sera ya Jinsia (2016).

Vilevile kuondoa dhamana kwa washtakiwa mpaka hukumu itakapotoka, lakini bado kesi za udhalilishaji na ukatili wa kijinsia zinaripotiwa na kwa mujibu wa Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar kesi 1,954 na asilimia 83.7 ikiwa ni za watoto na asilimia 12 ni wanawake.

Mama Mariam ameeleza katika juhudi za kuisadia Serikali kulimaliza kabisa tatizo hili, taasisi ya ZMBF wamefanya mambo makubwa ikiwemo; kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuandaa mfumo wa kidijitali wa kukusanya kanzi data ya takwimu za taarifa za matukio ya ukatili na udhalilishaji.

Pia, kuzindua Kampeni ya Kimataifa ya Jumuiya wa Madola inasema Sasa Basi kwa ukatili wa kingono na majumbani, kutoa elimu kwa kamati za jinsia zilizopo katika Shehia, kufanya midahalo na wanajamii.
Jambo la mwisho ni kuandaa makazi salama maalum kwa ajili ya waathirika wa udhalilishaji na ukatili wa kijinsia hususan wanawake na watoto kuwapatia msaada wa huduma za afya ya akili.

Sambamba na msaada wa kisheria na mafunzo ya ujuzi wa kistadi ili waweze kuwa na vyanzo vya kujipati kipato pale watakaporudi katika jamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news