Mama Mariam Mwinyi awasili nchini Marekani kushiriki mikutano ya OAFLAD

NEW YORK-Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mhe. Mama Mariam Mwinyi, ameondoka Zanzibar na kuwasili New York, Marekani, tarehe 20 Septemba 2024, kuiwakilisha Tanzania katika mikutano iliyoandaliwa na Taasisi ya Wake wa Marais Barani Afrika (OAFLAD), itakayofanyika New York kuanzia Septemba 21 hadi Septemba 26, 2024.
Mkutano huo utajadili uwekezaji na utekelezaji wa afua jumuishi za kijamii, hususan afya na elimu kwa watoto na wasichana.

Aidha Mikutano hiyo itafanyika sambamba na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNGA), ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mama Mariam Mwinyi amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Elsi Kanza, pamoja na Balozi Dkt. Suleiman Haji Suleiman, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F. Kennedy.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news