MANYARA-Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura limehitimishwa hii leo tarehe 10 Septemba,2024 kwa mikoa ya Manyara, Simiyu na Mara huku mwitikio wa Wananchi ukionekana kuwa mkubwa katika zoezi hili.
Zoezi hili la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura umedumu kwa siku saba na ulianza tarehe 04 Septemba, 2024 huku lilibebwa na Kauli mbiu isemayo "Kujiandikisha kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora"