Manyoni waipongeza TEA kwa miradi ya elimu

DODOMA-Mbunge wa Manyoni Mashariki mkoani Singida, Mhe. Dkt. Pius Chaya aimepongeza Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia hapa nchini.
Mbunge wa Manyoni Mashariki,Mhe. Dkt. Pius Chaya (kushoto) akifafanua jambo kuhusu miradi ya elimu alipomtembelea Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Dkt. Erasmus Kipesha ofisini kwake jijini Dodoma.

Akizungumza Septemba 13, 2024 katika ofisi za TEA jijini Dodoma, Dkt. Chaya amesema, ameshuhudia miradi mingi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo, mabweni, nyumba za walimu pamoja na maktaba za sayansi ambazo zimejengwa na TEA.

Dkt. Chaya amemtembelea Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Dkt. Erasmus Kipesha ofisini kwake kwa lengo la kutoa shukrani kwa miradi ya elimu jimboni kwake ambayo amesema imesaidia katika kuinua ubora wa elimu.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu ya Elimu Tanzania (TEA), Dkt. Erasmus Kipesha (Kulia) akielezea utekelezaji wa miradi ya elimu unavyofanyika wakati alipotembelewa na Mbunge wa Manyoni Mashariki, Mhe. Dkt. Pius Chaya jijini Dodoma.

"Jimboni kwangu Manyoni Mashariki ni wanufaika wa miradi inayotekelezwa na TEA hivyo nimekuja pamoja na diwani kuwashukuru sana kwa miradi hiyo,"amesema Dkt. Chaya.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Dkt. Erasimus Kipesha (Kulia) akimsikiliza Mhe. Dkt. Pius Chaya mbunge wa Manyoni Mashariki alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma.

Ameitaja miradi ya elimu ambayo imefadhiliwa na TEA jimboni Manyoni Mashariki kuwa ni ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari Sasajila, vyumba vitatu vya madarasa shule ya msingi Sanza na Kintinku pamoja na matundu 24 ya vyoo shule ya msingi Kintinku.
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Dkt. Erasmus Kipesha (Kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Dkt. Pius Chaya mbunge wa Manyoni Mashariki (wa pili kulia), Ezekiel S. Ezekiel Diwani Kata ya Nkonko Manyoni (wa tatu kuli) pamoja na Masozi Nyirenda, Kaimu Mkurugenzi Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi TEA ( kushoto).

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Dkt. Erasmus Kipesha amemshukuru Mbunge huyo kwa kusimamia vizuri utekelezaji wa miradi hiyo hadi imekamilika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news