Mapendekezo ya marekebisho ya sheria nane yawasilishwa bungeni

DODOMA-Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza Johari amewasilisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 2) wa Mwaka 2024 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 2) Bill, 2024].
Muswada huo umewasilishwa mbele ya Bunge la Jamhuri ya Tanzania tarehe 3 Septemba, 2024 bungeni jijini Dodoma.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema, muswada huo unalenga kufanya Marekebisho katika Sheria kuu nane ambazo ni; Sheria ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu Sura ya 432 ( The Anti- Trafficking in Person Act, Cap 432),
Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai Sura ya 20 ( The Criminal Procedure Act, Cap 20), Sheria ya Serikali Mtandao Sura ya 273 (The e-Government Act, Cap 273) Sheria ya Uhamiaji Sura ya 54 ( The Immigration Act, Cap 54),

Sheria ya Ardhi Sura ya 113 (The Land Act, Cap 113), Sheria ya Bohari ya Dawa 70 ( The Medical Stores Department Act, Cap 70) Sheria ya Viwango Sura 30 ( The Standard Act, Cap 30) na Sheria ya Tume ya Mipango Sura ya 127 ( The Planning Commission Act, Cap 127).
Akiwasilisha muswada huo, Mhe. Johari amesema Sheria ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu Sura ya 432, ambayo ilitungwa Mwaka 2008 na mpaka sasa imeshafanyiwa marekebisho mara tano.

Amevitaja vifungu vilivyopendekezwa kufanyia marekebisho katika sheria hiyo kuwa ni kifungu cha 3,17,30 31 32, vilevile Sheria hiyo inapendekeza kuongezwa kwa vifungu vipya vya 24A, 24B, 24C, na 24D.
“Mhe. Naibu Spika marekebisho yaliyopendekezwa yanalenga kutatua changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa vifungu mbalimbali wa sheria hii na kuboresha vifungu hivyo ili kuimairisha Nyanza zote za kuzuia usafirishaji haramu wa binadamu.”

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameendelea kueleza kuwa Sheria ya Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai Sura ya 20, Sheria hii ilitungwa mwaka 1985 mpaka sasa imeshafanyiwa marekebisho mara 35, kifungu kinachopendekezwa kurekebishwa ni kifungu cha 205A kwa kuanisha namna muundo wa kuandaa ripoti ya uchunguzi wa Kifolensiki.
Aidha,Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema Muswada huo unapendekeza kufanyika kwa Marekebisho katika Sheria ya Serikali Mtandao Sura ya 273 iliyotungwa Mwaka 2019 na haijawahi kufanyiwa marekebisho,

Sheria hiyo imefanyiwa Marekebisho katika kifungu cha 57 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuongeza adhabu kwa kosa la kuondoa, kuharibu au kubadili data kumbukumbu za kielektroniki, mfumo au vifaa vya kielektroniki kwa lengo la Marekebisho haya ni kuhakikisha adhabu zinazowekwa zinazingatia uzito wa makosa.

Katika hatua nyingine Mhe. Johari ameitaja Sheria ya Uhamiaji Sura ya 54 ya Mwaka 1995 ambayo imefanyia marekebisho mara 12, Sheria hiyo imerekebishwa kwenye vifungu vya 3,20 23, 28, 32, 37, 46, 48 pia kuongezwa kwa kifungu kipya cha 8B na kifungu cha 42A, kifungu cha 11 kimepedekezwa kufutwa ili kuepusha mgongano wa kati ya Sheria ya Uhamiaji na Sheria ya Tume ya Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Idara ya Uhamiaji Tanzania.
Muswada wa huo unapendekeza kufanya Marekebisho katika Sheria ya Ardhi Sura ya 113, Sheria hii ilitungwa Mwaka 1999 na imefanyikwa marekebisho mara 14, kifungu cha 19 kinapendekezwa kufanyiwa marekebisho kwa lengo la kuweka utaratibu wa matumizi ya Ardhi kwa mtu aliepewa hadhi maalumu chini ya Sheria ya Uhamiaji, hata hivyo Serikali imependekeza marekebisho hayo kuondolewa ili yaendelee kufanyiwa kazi kwa kina zaidi.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali amezungumzia Marekebisho katika Sheria ya Bohari ya Dawa Sura ya 70 ya Mwaka 1993 ambayo imesharekebishwa mara 2, Muswada unapendekeza Marekebisho katika kifungu cha 16A, kwa lengo la kuongeza wigo wa uwekezaji wa Taasisi hiyo na kuiwezesha kujiendesha kibiashara kwa kuzingatia maelekezo yatakayokuwa yanatolewa na Msajili wa Hazina na Mamlaka nyingine zinazohusika.

Vilevile Muswada huo unaopendekeza kufanyiwa Marekebisho katika Sheria ya Viwango Sura ya 130 iliyotungwa Mwaka 2009 na kufanyiwa marekebisho mara 1, Marekebisho hayo yanalenga katika vifungu vya 2, 4, 21A, 22, 23, 24, 27, 36. Marekebisho ya Sheria hii yanalenga kuimarisha utendaji kazi wa Shrika la Viwango nchini.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameendelea kwa kueleza kuwa Sheria ya Tume ya Mipango Sura ya 127 iliyotungwa Mwaka 2023, na inafanyiwa Marekebisho kwa mara ya kwanza, Sheria hii inapendekezwa kwa ujumla katika masharti mbalimbali kwa kubadili jina la Tume na kuwa Tume ya Taifa ya Mipango kwa lengo la kuwianisha jina la Tume na wigo wa majukumu yake, pia kifungu cha 5 kimependekezwa kurekebishwa kwa kuongeza idadi ya wajumbe wanaoteuliwa na Rais kutoka wajumbe watano mpaka wajumbe nane.

Akimalizia katika kuwasilisha Muswada huo Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameliomba Bunge la Jamhuri ya Muunganio wa Tanzani kuujadili na kuupitisha katika hatua ya kusomwa kwa mara ya pili na tatu na baadae kupitishwa kuwa Sheria ya Nchi.
“Mhe. Spika baada ya maelezo haya kwa mujibu wa Kanuni ya 99 ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Mwaka 2023, ninaomba kutoa hoja kwamba Muswada huu wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.2) wa Mwaka 2024 [ The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No2) Bill, 2024], kama ulivyo rekebishwa kupitia jedwali la Marekebisho ujadiliwe na kupitishwa katika hatua kusomwa kwa mara ya pili na ya tatu na hatimae marekebisho yanayopendekezwa yawe sehemu ya Sheria ya Nchi”,

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news