Mara Sports Academy watwaa ubingwa Polisi Jamii Cup

MARA-Timu ya Mara Sports Academy imetwaa kombe la Polisi Jamii Cup baada ya kuibuka kidedea kwa kuifunga Mshikamano FC kwa bao 1-0.
Fainali ya mashindano ya Polisi Jamii Cup yalifanyika Septemba 29,2024 mkoani hapa ambapo,Mara Sports Academy, kama mshindi wa kwanza walijinyakulia zawadi ya ng'ombe mmoja na mipira miwili.

Mshindi wa pili, Mshikamano FC, walijinyakulia mbuzi mmoja na mipira miwili, huku mshindi wa tatu akiambulia mipira miwili.

Zawadi hizo zilikabidhiwa kwa manahodha wa timu zote na mgeni rasmi, alikuwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi wa Polisi Nenrad Sindano, ambaye alisisitiza umuhimu wa mashindano haya katika kuimarisha uhusiano kati ya jamii na Jeshi la Polisi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news