Mbunge Hassan Mtenga azidi kuwaheshimisha vijana Mtwara Mjini kupitia Mtenga Jimbo Cup

MTWARA-Ligi ya Mpira wa miguu (Mtenga Jimbo Cup) iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini, Mhe.Hassan Mtenga imefikia tamati Septemba 28,2024 kwa kishindo huku timu ya Mpira wa Miguu kutoka Kata ya Vigaeni ikifanikiwa kujinyakulia kombe na Shilingi 1,000,000.
Ni baada ya kufanikiwa kuwa mshindi wa kwanza kwenye mashindano hayo ikifuatiwa na timu ya Mpira wa Miguu kutoka Kata ya Chikongola iliyoshika nafasi ya pili na kujinyakulia shilingi 500,000.

Aidha,timu kutoka Naliendele ilijinyakulia shilingi laki mbili na elfu hamsini kwa kuwa mshindi wa tatu

Mhe. Mtenga amesema kuwa dhamira ya kuanzisha ligi hiyo ni kumuunga Mkono Mhe. Rais katika sekta ya michezo pamoja na kuibua vipaji vitakavyosaidia kuunda timu ya Mkoa itakayoshiriki ligi Kuu Tanzania Bara.
Amesema kuwa, tangu ligi ilipoanza imeibua vipaji vingi na mefanikinwa kuibua vipaji saba ambavyo watawasaidia kufanikisha malengo yao katika michezo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mtwara Mjini Salumu Naida amempongeza Mbunge huyo Kwa kuendelea kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa vitendo katika michezo

Katika ligi hiyo viongozi mbalimbali walipata wasaa wa kuhamasisha wananchi kushiriki Kwenye zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27,2024.
Fainali ya Mtenga Jimbo Cup awamu ya pili imefanyika katika Viwanja vya Nangwanada Sijaona.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news