Meya Ndile awataka wananchi Mtwara Mikindani kudumisha usafi

MTWARA-Mstahiki Meya wa Manispaa Mtwara-Mikindani, Mhe. Shadida Ndile amewataka wananchi wote wa Manispaa kuhakikisha wanafanya usafi katika maeneo yanayowazunguka ili kuepukana na magonjwa na kuimarisha afya.
Aidha, Ndile amewapongeza wafanya biashara wa Soko la Samaki feri kwa kutunza mazingira katika eneo hilo na kuwasisitiza kuendelea na desturi ya kufanya usafi ili kuendeleza kuimarisha afya ya mlaji.
Pamoja na hayo Mstahiki Meya amewasisitiza wananchi hao kuchagua viongozi bora watakao waletea Maendeleo katika mitaa yao Kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27,2024.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Rugembe Maiga amewashukuru wafanyabiashara wa soko hilo kwa kujitokeza kwa wingi kufanya usafi na amewasisitiza kuendelea kuyatunza na kuyasimamia mazingira ili yaweze kuleta ustawi wa maisha endelevu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news